Check Out "Nanje ndagukunda" ya Linias wa EBSS song and lyrics

Mshiriki wa EBSS 2012 Linias Mhaya ameachia wimbo wake wa kwanza unaitwa Nanje ndagukunda, angalia video hii ya Wimbo huo na Lyrics zake.

LULU KAPATA DHAMANA, kwa 20. Mil

Taarifa za uhakika nilizozipata kwa sasa ni kwamba kuna uwezekano mkubwa mwigizaji Lulu akatoka kwa dhamana kesho Tarehe 25.


Uhakika wa Lulu kupata dhamana ulikua jana jumatano lakini ikawa imeshindikana kutokana na kuahirishwa kwa sababu jaji alipata dharura na pia kiwango cha pesa za dhamana kilikua hakijatimia.

Chanzo cha kuaminika kimesema dhamana ya kumtoa Lulu ambae amekua chini ya ulinzi kuanzia April 2012 ni milioni 20 za kitanzania.

Lulu amekua akishikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mwigizaji Steven Kanumba tangu April 2012, endelea kuipitia abrangula.com kwa stori zaidi.

Keisha: Nimetumia zaidi ya 10. Mil. kufanya Video na Diamond "Nimechoka"

Ile picha iliyosambaa mtandaoni ikimuonyesha Diamond anajipaka poda ndani ya gari akiwa na msichana basi Script yake ilikuwa ya humu ndani, tizama video mpya ya Keisha akiwa na Diamonda track inaitwa nimechoka kupitia InfoGramme Blog.

Kuhusu Video hii Keysha amesema,  "Nimetumia zaidi ya shilingi za Tanzania Milioni 10 kuandaa video hii, hii ikiwa ni pamoja na malipo kwa AJ ambaye amesimamia kazi yote, video hii ilikuwa itoke muda mrefu lakini kutokana na msururu wa ratiba ya shoo za nje ya nchi nilijikuta mara kadhaa ninahirisha kushoot, nashukuru Mungu imekamilika na huu ni mwanzo wa mafanikio yangu katika mwaka huu wa 2013"

FID Q APEWA CHETI CHA HESHIMA KUTOKA UNDER THE SAME SUN

Mkali wa mashairi na flow kutoka Mwanza Fareed Qubanda a.k.a Fid Q ametunukiwa cheti maalum cha shukurani na shirika linalosaidia watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) linalojulikana ma "Under The Same Sun" kwa mchango wake mkubwa katika kusapoti kampeni ya shirika hilo.
Fid Q akikabidhiwa cheti na Mr. Ash
Fid Q amepost picha akiwa na mwanzilishi na mwenyekiti wa shirika hilo la Canada, Peter Ash, na kuisindikiza picha hiyo na maandishi yanayosomeka.. "Just received CERTIFICATE OF APPRECIATION from the one and only Mr. Peter Ash (CEO of Under The Same Sun)."

Mwaka jana Fid Q akiwa na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya na walizungukia mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahamasisha watu kupinga mauaji ya albino wakiwa na shirika hilo.

OFA KWA AJILI YAKO

Uongozi wetu wa El - Shaddai Record's, Tuliopo Maghorofani kituo cha marolli karibu na kituo cha mafuta. tumeamua kutoa OFA maalumu ktk msimu huu wa Siku kuu za X-Mas na Mwaka Mpya kwa kila Recording kuwa nusu gharama ya kawaida.
Hili limethibitishwa na Mkurugenzi wetu mkuu, George David, ya kuwa kila Recording itakuwa nusu ya gharama ya kawaida kwa msimu huu na  baadae kidogo kwa nyimbo (audio), Matangazo na kila kitu ikiwemo kazi ambazo hazikumaliziwa kutoka ktk studio nyingine.
Moja kati ya Mandhari zetu ndani ya Studio.
Na huu ni moja kati ya ujumbe ulioandikwa na CEO wetu ktk FaceBook.. "NATOA OFFER KURECORD KWA NUSU GHARAMA KWA MEMBER YOYOTE WA EL SHADDAI RECORDZ AMBAYE ANAIMBA MUZIKI WA AINA YOYOTE KTK MSIMU HUU WA X - MASS NA MWAKA MPYA.KARIBUNI SANA"..
Mawasiliano yetu ni 0752 513 276, Email: elshaddairecordz@gmail.com. Wote tunakaribishwa..
 
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU.