OFA KWA AJILI YAKO

Uongozi wetu wa El - Shaddai Record's, Tuliopo Maghorofani kituo cha marolli karibu na kituo cha mafuta. tumeamua kutoa OFA maalumu ktk msimu huu wa Siku kuu za X-Mas na Mwaka Mpya kwa kila Recording kuwa nusu gharama ya kawaida.
Hili limethibitishwa na Mkurugenzi wetu mkuu, George David, ya kuwa kila Recording itakuwa nusu ya gharama ya kawaida kwa msimu huu na  baadae kidogo kwa nyimbo (audio), Matangazo na kila kitu ikiwemo kazi ambazo hazikumaliziwa kutoka ktk studio nyingine.
Moja kati ya Mandhari zetu ndani ya Studio.
Na huu ni moja kati ya ujumbe ulioandikwa na CEO wetu ktk FaceBook.. "NATOA OFFER KURECORD KWA NUSU GHARAMA KWA MEMBER YOYOTE WA EL SHADDAI RECORDZ AMBAYE ANAIMBA MUZIKI WA AINA YOYOTE KTK MSIMU HUU WA X - MASS NA MWAKA MPYA.KARIBUNI SANA"..
Mawasiliano yetu ni 0752 513 276, Email: elshaddairecordz@gmail.com. Wote tunakaribishwa..
 
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU.

Rest In Peace SHARO BILLIONEA

Msanii, Muigizaji, Mchekeshaji Hussein Ramadhani aka Sharo Bilionea amepata ajali ya gari akiwa anaendesha mwenyewe Toyota Harrier akitoka Dar kwenda Muheza kwao.
Baada ya Ajali (Samahani kwa picha hii)
Sharo Milionea ambaye alitamba sana kwenye filamu ya vichekesho ya Mzee Majuto ya Back From New York ambayo aliigiza kama "Sharobaro" amefariki dunia leo baada ya kupata ajali ya gari.
Sharo Milionea ambaye jina lake halisi ni Hussein Ramadhani alifariki dunia kufuatia gari lake kupinduka mara kadhaa baada ya kuacha njia.

Kamanda wa polisi wa Tanga, Afande Constatine Masawe akithibitisha kifo hicho alisema "Leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”.

Elshaddai.blogspot.com inawapa pole ndugu na jamaa wa marehemu na watanzania kwa ujumla kwa kuondokewa na msanii huyu ambaye alijizolea sifa nyingi kutokana na kipaji chake kwenye sanaa na alikuwa kipenzi cha wengi.

Mungu ailze roho yake mahali pema peponi. AMEEN...

FRED MTOI WA BBC AFARIKI DUNIA

Mtangazaji wa BBC, Afrika Fred Mtoi amefariki dunia.

Fred alianza kazi ya utangazaji katika redio Tanzania kabla ya kwenda Ulaya katika mafunzo..
Fred Mtoi
Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu kimoja cha London.

Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.

Alishiriki piya katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.

Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.

Matayarisho yanafanywa kusafirisha mwili wake hadi Tanzania.



BEN POL: NATAKA COLLABO NA WALTER

Msanii Ben Paul aliyeimba wimbo uliompa ushindi Walter wa Epic BSS amesema Alishaongea na Walter wakati wa kujitayarisha kwa ajili ya show ya fainali na kusema alimwambia Angependa kufanya kazi na Walter akiwa tayari kufanya kazi muda wowote.


Kwasasa ameshinda so achukue muda wake kujipanga ukizingatia kwa sasa watu wakaribu naye watakuwa wakimshauri sana.
BEN POL AKIMTUZA wALTER WAKATI ANAIMBA NIKIKUPATA NYIMBO YAKE.
Ila fahamu kuwa Ben Paul yupo tayari kufanya wimbo na Walter muda wowote.

Pia kuhusu Walter kuchagua `Nikikupata' kama wimbo wake wa mwisho kuimba nikitu kilicho mfurahisha sana Ben Paul na Ben amesema walivyo kuwa Back Stage Walter alimwambia ataimba wimbo huo kwenye show yake so Ben Paul alibidi autoe wimbo huo kwenye orodha ya nyimbo alizo taka kufanya kwenye show yake.
Kuhusu show aliyo fanya Ben Paul kwenye Epic BSS, Ben amesema tayari washindani walikuwa wamekaa kwenye mafunzo na walikuwa wanajua kufanya show nzuri ila kila msanii anauwezo tofauti na alichotaka kufanya nikuwaonyesha vitu na maujanja zaidi kwenye show ile ili wajifunza na waondoke na mambo tofauti kutoka kwa Ben Paul..

WALTER CHILAMBO: Mshindi EBSS 2012

Ben Pol akimtunza Walter kabla ya kumpa Saluti
Walter akiwa na mshindi wa pili Salma wakisubiri kutangazwa mshindi
Walter akimkumbatia Madam Rita baada ya kutangazwa mshindi
Akiwajibika siku ya FINAL
Walter akikabidhiwa pesa zake.
Zantel wamempa Big UP

OUR PRODUCER: George David

George David
Hallow watanzania wa Mbeya the Green city, hii ni mpya  na ya kipekee.

Hii ndo ile studio kwa ajili ya Audio zenye Quality ya juu nyanda za juu kusini ikiwa chini ya mzoefu wa Music George David.
Tunapatikana maeneo ya Magorofani karibu na kituo cha mafuta nyuma ya magari makubwa (maroli)