FID Q APEWA CHETI CHA HESHIMA KUTOKA UNDER THE SAME SUN

Mkali wa mashairi na flow kutoka Mwanza Fareed Qubanda a.k.a Fid Q ametunukiwa cheti maalum cha shukurani na shirika linalosaidia watu wenye ulemavu wa ngozi(albino) linalojulikana ma "Under The Same Sun" kwa mchango wake mkubwa katika kusapoti kampeni ya shirika hilo.
Fid Q akikabidhiwa cheti na Mr. Ash
Fid Q amepost picha akiwa na mwanzilishi na mwenyekiti wa shirika hilo la Canada, Peter Ash, na kuisindikiza picha hiyo na maandishi yanayosomeka.. "Just received CERTIFICATE OF APPRECIATION from the one and only Mr. Peter Ash (CEO of Under The Same Sun)."

Mwaka jana Fid Q akiwa na wasanii wengine wa muziki wa kizazi kipya na walizungukia mikoa ya kanda ya ziwa na kuwahamasisha watu kupinga mauaji ya albino wakiwa na shirika hilo.

No comments:

Post a Comment