Msanii, Muigizaji, Mchekeshaji Hussein Ramadhani aka Sharo Bilionea
amepata ajali ya gari akiwa anaendesha mwenyewe Toyota Harrier akitoka
Dar kwenda Muheza kwao.
Sharo
Milionea ambaye alitamba sana kwenye filamu ya vichekesho ya Mzee Majuto
ya Back From New York ambayo aliigiza kama "Sharobaro" amefariki dunia
leo baada ya kupata ajali ya gari.
Baada ya Ajali (Samahani kwa picha hii) |
Sharo Milionea ambaye jina
lake halisi ni Hussein Ramadhani alifariki dunia kufuatia gari lake
kupinduka mara kadhaa baada ya kuacha njia.
Kamanda wa polisi wa Tanga, Afande Constatine Masawe akithibitisha kifo hicho alisema "Leo majira ya saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera Muheza mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”.
Elshaddai.blogspot.com inawapa pole ndugu na jamaa wa marehemu na watanzania kwa ujumla kwa kuondokewa na msanii huyu ambaye alijizolea sifa nyingi kutokana na kipaji chake kwenye sanaa na alikuwa kipenzi cha wengi.
Mungu ailze roho yake mahali pema peponi. AMEEN...