FRED MTOI WA BBC AFARIKI DUNIA

Mtangazaji wa BBC, Afrika Fred Mtoi amefariki dunia.

Fred alianza kazi ya utangazaji katika redio Tanzania kabla ya kwenda Ulaya katika mafunzo..
Fred Mtoi
Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu kimoja cha London.

Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.

Alishiriki piya katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.

Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.

Matayarisho yanafanywa kusafirisha mwili wake hadi Tanzania.



No comments:

Post a Comment